Rais Biden amekamilisha mkutano wa NATO akiuita ni wa kihistoria

Rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano wa NATO mjini Vilnius, Lithuania.

Mkutano huo wa siku mbili katika mji mkuu wa Lithuania ulishuhudia uungwaji mkono mpya kwa Ukraine kujiunga na muungano huo lakini haukuweka muda maalum ambao Ukraine iliuhitaji.

Rais Joe Biden amehitimisha kile alichokielezea kama mkutano wa kihistoria wa NATO na matumaini ya kutatua mzozo wa Ukraine na onyo kali kwa Moscow.

Mkutano huo wa siku mbili katika mji mkuu wa Lithuania ulishuhudia uungwaji mkono mpya kwa Ukraine kujiunga na muungano huo lakini haukuweka muda maalum ambao Ukraine iliuhitaji.

“Hatutayumba,” Biden alirudia mara mbili wakati akizungumza na umati wa maelfu ya watu waliokusanyika katika Chuo Kikuu cha Vilnius, taasisi iliyopo kwa karne 4 ambayo imepitia uvamizi wa taifa la Baltic wa vikosi vya Poland, Russia, Sovieti na Ujerumani. “Nia yetu ya dhati kwa Ukraine haitadhoofika,” Biden alisema. “Tutasimama kwa umoja na uhuru, leo, kesho na kwa muda mrefu kama inavyohitajika.”

Pia alitoa onyo kali kwa Rais wa Russia Vladimir Putin. Kwa bahati mbaya, Russia haijaonyesha nia ya kutaka suluhu la kidiplomasia. Putin bado anaamini anaweza kuishinda Ukraine. Hawezi kuamini kuwa ni ardhi yao, nchi yao, mustakbali wao wa baadae. Na hata baada ya wakati huu wote, Putin bado ana shaka juu ya nguvu zetu za kuendelea kuwepo madarakani. Bado anafanya kazi mbaya,” alisema Biden.