Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watu hao walitekwa nyara baada ya watu wenye bunduki kuuvamia msafara wao kwenye eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta, hapo Desemba 12, ambapo wanajeshi wanne waliokuwa wakiwalinda waliuwawa, pamoja na madereva wawili ambao ni raia wa kawaida.
Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini kwenye taarifa yake kwamba watu hao walioachiliwa wako kwenye hali nzuri ya kiafya, na kwamba baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya, wamepelekwa kwenye eneo salama, na pia walipata nafasi ya kuzungumza na jamaa zao.
Mashambulizi ya wanamgambo kwenye eneo la Niger Delta yamepungua katika miaka ya karibuni, ingawa eneo hilo linaendelea kushuhudia wizi mkubwa wa mafuta ghafi, pamoja na uharibifu kwenye mabomba ya mafuta, hali iliyoathiri pakubwa uzalishaji mafuta nchini Nigeria.