Putin ameweka nyaraka zinazoelezewa na Uingereza kama "Historia ya Silaha"

Rais wa Russia, Vladimir Putin akiwa Moscow, Russia. Nov. 8, 2023.

Katika taarifa ya kijasusi ya Jumamosi kuhusu Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasema uchapishaji wa Putin ni mkusanyiko wa nyaraka 242 zenye kichwa cha habari “Katika umoja wa kihistoria wa raia Wa-Russia na Wa-Ukraine”. Nyaraka hizo kutoka karne ya 11 hadi karne ya 20

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inaripoti kuwa Rais wa Russia, Vladimir Putin na Rais wa zamani nchini humo Dmitry Medvedev wametoa nyaraka zilizoelezewa na wizara ya Uingereza kama “historia ya silaha , iliyolenga kukabiliana dhidi ya dhana za Magharibi katika akili za watu wa Russia na kuwatisha majirani zake walio karibu wa magharibi”.

Katika taarifa ya kijasusi ya Jumamosi kuhusu Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasema uchapishaji wa Putin ni mkusanyiko wa nyaraka 242 zenye kichwa cha habari “Katika umoja wa kihistoria wa raia Wa-Russia na Wa-Ukraine”. Nyaraka hizo kutoka karne ya 11 hadi karne ya 20, ni jaribio la Putin kuhalalisha sera ya sasa ya Kremlin kwa Ukraine na inaelezea maoni ya kitafsiri kutoka kwa rais.

Chapisho la Medvedev ni makala ambayo wizara ya Uingereza inasema aliandika kwa uwazi kuhusu historia ya uhusiano wa Russia na Poland. Anaishutumu Poland kwa kujihusisha na sera ya ukandamizaji ya Russophobic, kulingana na wizara ya Uingereza na Medvedev anaitishia Poland kwa shambulio la kijeshi.

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, akiendelea kupigana na uvamizi wa Russia nchini mwake alitoa hotuba ya matumaini Ijumaa kabla ya Mkutano wa Amani wa Paris-Paris Peace Forum.