Papa Francis ahutubia Baraza la Congress

Papa Francis akiwapungia mkono maelfu ya watu nje ya jengo la Capitol Hill.

Papa Francis Alhamisi ametoa wito kwa bunge la marekani na wananchi wa taifa hilo kuweka pembeni tofauti zao na kurudisha upya roho ya urafiki na umoja , ukarimu na kushirikiana pamoja kwa maslahi ya kujipatia mambo mazuri..

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki ni wa kwanza kulihutubia bunge la Marekani na alishangiliwa sana kila wakati alipozungumzia masuala muhimu ya kijamii katika hotuba yake iliochukua dakika hamsini katika jengo la Capitol Hill.

Hotuba yake ilipeperushwa moja kwa moja na vyombo vya habari huku kukiwa na video kubwa nje ya jengo hilo amapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika. Baada ya kumaliza hotuba yake ndani ya bunge, baba Mtakatifu Francis alisimama nje na kuwapungia mkono maelfu ya watu waliokuwa wakimshangilia.