Polisi wawili na raia mmoja wauwawa na kundi la Al Shabab Kenya

Wanamgambo wa Alshabab washambulia garai la Polisi mashariki mwa Kenya.

Wapiganaji wa Al Shabaab wameshambulia gari la polisi mashariki mwa Kenya na kuwaua maafisa wawili na raia mmoja, polisi na kundi hilo lenye silaha wamesema.

Lori hilo lilikuwa likisafiri kutoka kambi ya Hayley Lapsset kuelekea mji wa Garissa, karibu kilomita 120 kutoka mpaka wa Somalia, wakati lilipokanyaga kifaa cha mlipuko, polisi walisema katika taarifa jana Jumatano.

Wanamgambo hao halafu walirusha guruneti kwenye gari hilo na kuingia katika mapigano makali ya risasi ambayo yalichukua maisha ya waathirika, polisi walisema.

Radio Andalus ya Al Shabaab ilisema katika matangazo yake kuwa watu wao waliokuwa na silaha waliwaua askari wawili wa Kenya na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulio hilo.