Polisi wa Israel wamewafyatulia risasi washambuliaji huko Ukingo wa Magharibi

Polisi wa Israeli wakiwa kwenye kituo cha ukaguzi cha Ras Biddu huko Ukingo wa magharibi. January 7, 2024.

Tukio hilo limetokea saa chache baada ya watu tisa kuuawa katika ghasia nyingine kwenye eneo hilo linalokaliwa kimabavu  na Israel

Polisi wa Israel siku ya Jumapili waliwafyatulia risasi washambuliaji wawili wanaoshukiwa walivurumisha gari lao katika kituo cha ukaguzi huko Ukingo wa Magharibi, na kumuua msichana wa Ki-palestina katika gari lililokuwa karibu, kulingana na polisi pamoja na maafisa wa afya.

Washukiwa hao wawili pia walipigwa risasi, wakati afisa wa polisi kijana alijeruhiwa kiasi. Tukio hilo la Jumapili jioni limetokea saa chache baada ya watu tisa kuuawa katika ghasia nyingine kwenye eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel, ambalo limeshuhudia ongezeko la ghasia tangu vita vya Israel dhidi ya Hamas vilipozuka Oktoba 7.

Polisi wa Israel wamesema mashambulizi hayo yalifanyika katika kituo cha ukaguzi karibu na kijiji cha Palestina cha Biddu, kilichopo kaskazini magharibi mwa Jerusalem. Picha za kamera za usalama zilionyesha gari jeupe likielekea kwa polisi wa Israel katika kituo cha ukaguzi. Kisha Polisi walilifuatilia gari hilo na kulifyatulia risasi.