Polisi Ujerumani yavamia maeneo ya Hamas na Samidoun

Polisi wa Ujerumani wakiwa nje jengo walilovamia wakati wa msako dhidi ya watu wanounga mkono Hamas.Novemba 23,2023. REUTERS.

Polisi nchini  Ujerumani ilifanya uvamizi Alhamisi kuhusiana na kundi  la wanamgambo ambalo lilipigwa marufuku la Hamas na kundi linalounga mkono Palestina  la Samidoun.

Polisi nchini Ujerumani ilifanya uvamizi Alhamisi kuhusiana na kundi wa wanamgambo ambalo lilipigwa marufuku la Hamas na kundi linalounga mkono Palestina la Samidoun.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani ilisema uvamizi huo ulifanyika katika maeneo 15 katika majimbo manne.

Kwa kupigwa marufuku Hamas na Samidoun nchini Ujerumani, tumetuma ishara za wazi kwamba hatutavumilia kutukuzwa au kuunga mkono ugaidi wa kinyama wa Hamas dhidi ya Israeli, Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser alisema katika taarifa yake.

Wizara hiyo inasema kuna takriban wanachama 450 wa Hamas nchini Ujerumani na kwamba wameshiriki katika propaganda na juhudi za kutafuta fedha.