Polisi DRC watumia gesi  kesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji

Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametumia gesi  kesi ya kutoa machozi ili kutawanya waandamanaji katika mji mkuu kinshasa.

Maandano hayo yaliitishwa na upinzani uliokuwa ukijimuhisha aliyekuwa waziri mkuu Matata Ponyo, Martin Fayulu, Moise Katumbi na Delly Sesanga wananuia kukemea gharama ya juu ya maisha ya kawaida, ukosefu wa usalama Mashariki mwa DRC na hali ya kutoweka wazi katika maandalizi ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Majadiliano yalikumbwa na vurugu pale wafuasi wa upinzani walipokataa kufuata mwongozo uliowekwa na serikali wakisema kuwa si wa haki na unalenga kuwazuia ili wasiandamane.

Martin Fayulu amesema kuwa hali ya polisi kutawanya wanaoandamana inadhiirisha wazi kwamba serekali ya Felix Tshisekedi imeshindwa kutekeleza sera yake ya kukuza haki na sheria kama inavyosema katiba ya nchi nakulahumu polisi kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Gavana wa mkoa wa Kinshasa, Gentini Ngobila pia amelaumu upinzani kutaka kuvuruga usalama wa umma.

Katika purukushani hizo zaidi ya watu saba wamejeruhiwa wakiwemo askari polisi watu pamoja na waandamanaji. Hata hivyo hakujawa na tangazo lolote kutoka kwa serikali.