Pence aitwa na jopo la mahakama Linalo- chunguza uvamizi wa bunge la Marekani

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence.

Mahakama ya Rufaa ya Serikali Kuu ya Marekani Jumatano ilimtaka  Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Mike Pence kufika mbele ya jopo la mahakama  linalochunguza kutengua matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 na kukataa ombi la mawakili wa rais wa zamani Donald Trump kuzuia ushahidi. 

Haikuwekwa wazi ni lini Mike Pence atafika mbele ya jopo hilo.

Kwa miezi kadhaa jopo hilo la mahakama limekuwa likifanya uchunguzi kufuatia tukio la Januari 6 mwaka 2021 , la uvamizi katika jengo la bunge la Marekani na juhudi za Trump na washirika wake kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

FILE - Mtu akiwa amevaa fulana yenye maandishi QAnon akikabiliana na afisa polisi wa Bunge la Marekani ndani ya Baraza la Seneti Washington, Jan. 6, 2021.

Lakini ushahidi wa Pence unakuja wakati akisogea karibu kufikia kinyang’anyiro cha urais wa mwaka 2024.

Huu utakuwa ni wakati muhimu wa kihistoria katika uchunguzi huo kuhusu uchunguzi huo na huenda ukawapa waendesha mashtaka maelezo ya mtu muhimu wa kwanza wakati wanaposonga mbele na uchunguzi huo.

Wakili wa Pence na msemaji wa Trump hawakurudisha haraka barua pepe zilizotaka maelezo, na msemaji wa baraza maalumu katika wizara ya sheria anayeongoza uchunguzi huo alikataa kutoka maelezo.