Wanaharakati wa Afrika wanapongeza uamuzi wa Papa wa kuwaruhusu makasisi wa Kikatoliki kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, wakiwa na matumaini kwamba ishara ya Papa inaweza kupunguza hisia za chuki dhidi ya LGBTQ na ukandamizaji barani humo. Lakini mashirika ya kidini ya Kiafrika hayatarajiwi kukubali tangazo la Vatican.
Mwanaharakati wa Nigeria Promise Ohiri, anayejulikana kama Empress Cookie, aliamka na kushangilia habari hii siku ya Jumanne.
Papa Francis amewataka mapadri wa kanisa Katoliki kuwabariki wapenzi wa jinsia moja katika tangazo lake la kihistoria.
Ohiri, muumini wa kikatoliki aliyebadili jinsia yake, anakabiliwa na ubaguzi mkubwa na vitisho kwa maisha yake kutokana na hali ya jinsia yake.
Anasema kwamba hakuwa na matumaini ya kupata habari bora lakini anakiri kuwa kutakuwa na upinzani.“Halitakuwa jambo rahisi. Nina uhakika kabisa kwamba Wa-Afrika wataandamana dhidi ya hili. Kwa kiasi kikubwa wanatumia dini dhidi yetu, watu wa aina hii. Nahisi kama Papa anafanya uamuzi huo, nahisi kama ni vizuri kwa watu wa aina hii. Nina hisia nzuri juu ya hilo”.
Vatican imesema kuwa baraka hizo hazitafanana na ibada ya harusi, ambayo inaendelea kufahamika inatokea tu, kati ya mwanamume na mwanamke.
Vatican imesema kuwa ushoga “umevuruga imani” lakini ikasisitiza kuwa wapenzi wa jinsia moja wanapaswa kuhudumiwa kwa upendo na heshima.
Lakini tangazo hilo limezua mijadala barani Afrika, ambako ushoga unatazamwa kwa kiasi kikubwa kama dhambi, chukizo, au kuiga utamaduni wa magharibi.
Nchini Nigeria, watu wenye uhusiano wa jinsia moja wanaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 14 jela.
Ohiri ana matumaini kuwa tangazo la Papa litabadilisha mambo.
“Papa kufanya hivyo ameishtua dunia nzima na amevunja misingi. Namaanisha, sheria nyingi ambazo zinawapinga watu wa aina hiyo. Kama dini hiyo inaunga mkono mashoga, niamini, itatikisa sheria ya Nigeria na nchi nyingine ambazo hazijatia saini kuwa sheria. Ni jambo la kawaida kwao kuandamana”.
Lakini Askofu John Promise Daniel, Makamu wa Rais wa Pentekoste Fellowship of Nigeria, anasema baraka za jinsia moja, au ndoa, hazikubaliki. “Mimi nipo juu au chini, kama vile, nilipata mshtuko wakati niliposikia kile Papa alichosema. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha msimamo wa neno la Mungu, iwe wewe ni papa, askofu mkuu, au chochote. kama neno la Mungu katika Biblia haliungi mkono, sijali mtu yeyote anayeunga mkono. Ni batili, uhuru wa mwanadamu hauendani”.
Kanisa Katoliki la Nigeria bado halijajibu amri ya Vatican.
Lakini wataalamu wanatabiri kwamba maafisa wa Kanisa Katoliki nchini Nigeria huwenda wasikubaliana na kuendelea na mafundisho tofauti juu ya suala hilo.
Mike Umoh, msemaji wa jamii ya Kikatoliki nchini Nigeria, alizungumza na VOA kwa njia ya simu.“Ninaweza kuwaambia kwamba maaskofu wa Kikatoliki wa Nigeria kwa sasa wanafanya kazi kwa nafasi yao ambayo itatangazwa hivi karibuni”.
Wiki hii, mahakama ya Uganda ilianza kusikiliza kesi inayopinga sheria kali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki dhidi ya LGBTQ, ambayo inawaadhibu “wanaojihusisha na ushoga” kifungo cha maisha.
Wanaharakati kama Ohiri wanasema wana wasiwasi kwamba sheria za Nigeria dhidi ya ushoga zitabatilishwa, lakini tamko la Papa ni hatua katika mwelekeo sahihi.