Papa Francis aomba serikali zisitishe safari hatari za wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranean

Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis kwenye picha ya maktaba.

Mkuu wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis Jumapili ameomba serikali zisitishe usafirishaji haramu wa binadamu kweye bahari ya Mediterranean.

Hayo amesema wakati akieleza huzuni yake kutokana na ajali ya boti ya wiki iliyopita karibu na ufukwe wa Italy wa Calabrian, ambapo darzeni ya watu walikufa. Wakati akitoa hotuba yake kwenye bustani za St Peter’s mjini Vatican, Papa Francis alisema kwamba,” Natoa wito wangu tena wa kuzuiliwa kwa matukio kama hayo .

Tunaomba walanguzi haramu wa binadamu wakomeshwe.” Mamlaka za kieneo zimesema kwamba kufikia sasa, miili 70 imepatikana kufutia ajali hiyo. Wahamijai waliokuwa kwenye boti iliyopata ajali wanasemekana kutokea Uturuki wengi wakiwa ni raia wa Afghanistan, Pakistan, Iran, Somalia na Syria.

Takriban watu 80 walinusurika kwenye ajali hiyo karibu na mgahawa wa kitalii wa Steccato di Cutro, karibu na ufukwe kwa Calabria mashariki mwa Italy. Boti hiyo inakisiwa kubeba watu 200 kabla ya ajali hiyo kutokea.