Papa Francis akamilisha ziara yake Hungary akitoa wito wa upendo na amani kwa jamii

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani

Ni furaha kubwa na ninaona faraja yenye nia ya dhati ya kujitolea kwa kuziangalia nyuso za watu”, alisema mhudhuriaji na muumini Laszlo Vuncs wakati akisubiri kuwasili kwa Papa Francis.

Maelfu ya watu walijaa uwanja wa Budapest siku ya Jumapili kuhudhuria misa ya umma na Papa Francis ambaye anahitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Hungary.

“Ni furaha kubwa na ninaona faraja yenye nia ya dhati ya kujitolea kwa kuziangalia nyuso za watu”, alisema mhudhuriaji na muumini Laszlo Vuncs, wakati akisubiri kuwasili kwa Papa Francis.

Papa Francis aliwasili uwanjani kwa gari lake maarufu wa “Popemobile” wakati umati wa watu ukimshangilia katika uwanja mkuu wa Kossuth mjini Budapest.

Peter Szoke, kiongozi katika jumuiya ya kiimani ya Sant’ Egidio huko Hungary ambaye alihudhuria misa hiyo alikubaliana na maagizo ya Papa.

Wito wa Jumapili wenye msisitizo ilikuwa mara ya pili kwa Papa Francis kutumia muktadha wa kidini kutoa maoni yake kuhusu wahamiaji.