Rais Obama: Wanawake wa Afrika wana mchango mkubwa kwa maendeleo

Rais wa Marekani, Barack Obama akipokea maua kutoka kwa msichana mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Julai 24, 2015.

Rais Barack Obama amesema kiashiria kizuri cha maendeleo katika taifa lolote ni jinsi linavyowatendea wanawake akiongezea kuwa wanawake wanapopatiwa huduma nzuri za afya na elimu, familia zinakuwa zenye nguvu, jamii zinashamiri na mataifa yanafanikiwa zaidi.

"Bara la afrika ni zuri, lina wanawake wenye nguvu. Jambo moja ambalo ni jema kabisa ni pale taifa linapofanikiwa kwa jinsi linavyowatenda vizuri wanawake wake. Wakiwapatia huduma nzuri za afya na elimu, na hili linajidhihirisha katika kuwa na jamii na taifa lenye mafanikio makubwa," amesema Rais Obama.

Amesema ukitaka kuwawezesha zaidi wanawake akizungumzia wanawake wa afrika rais obama amesema marekani itakuwa mshirika wao wa kweli. Na kuwasihi wafanye kazi pamoja katika kutokomeza manyanyaso ya kingono na majumbani .

Rais Obama amesema hakuna atakayestahimili uwabakaji utumike kama silaha ya vita, ni uhalifu na wale wanaotenda uhalifu ni vyema wawajibishwe na kuadhibiwa vikali.

Katika suala la viongozi wanawake amesema mwelekeo uwe katika kusisitiza kukiinua kizazi kijacho ili wapatikane viongozi wanawake ambao watasaidia katika mapambano ya kisheria na kusukuma mbele amani na wakati huo huo kufungua njia kwa biashara na milango ya ajira na kuajiri wote wanaume na wanawake.

Katika kile ambacho anadhani kimechangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake barani afrika, rais obama ametaja suala la kuziacha tamaduni za zamani ziingilie kati katika kuwaendeleza wanawake na kusema wakati umefika kwa kuangalia dunia inavyosonga mbele kimaendeleo.

Wakati wasichana wa kiafrika wanapokabiliwa na ukeketaji au kulazimishwa kuolewa mapema, hiyo inarudisha nyuma maendeleo na hili ni vyema likome amesisitiza rais Obama.

" Mimi kama baba mwenye watoto wawili wa kike naamini kuwa wana kila haki ya kupewa fursa ya kutimiza ndoto zao, na hilo liwe hivyo hivyo kwa wasichana walioko hapa Afrika. Hatuwezi kuruhusu tamaduni za zamani ziingilie kati kuzuia ndoto hizo," amesema rais.

Your browser doesn’t support HTML5

Obama asema wanawake wasiachwe nyuma

Kuhusiana na suala la ukimwi amesema asilimia 80 ya kesi mpya za hiv barani Afrika ni kwa wasichana na hilo ni janga ambalo linarudisha nyuma maendeleo. Amesema marekani inaanzisha ushirika na mataifa kumi ya afrika, tanzania, kenya, Uganda, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe ili kuwafanya wasichana wawe katika hali salama na wasio na ukimwi.

Amesema wakati wasichana wanaposhindwa kwenda shule na kukua wakiwa hawajui kusoma na kuandika, hiyo ni kuwanyima fursa ya kuwa wahandisi na marais wa baadaye na hilo linawarudisha nyuma. Mchango wa marekani kwa elimu na afya na wasichana rais obama amesema mke wake michelle anaongoza kampeni ya ulimwengu ikijumuisha tanzania na Malawi kwa kupeleka ujumbe rahisi kwamba tuwaache wasichana wetu wasome na wakue wakiwa na afya njema na wenye nguvu.

Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kila mmoja ana haki sawa, na kila mmoja ana thamani.Tunapoheshimu uhuru wa wengine, bila ya kujali rangi zao, wanavyoabudu au wao ni kina na wanampenda nani tutakuwa huru zaidi. Hadhi yangu inategemea yako na hadhi yako kadhalika inategemea yangu mimi.