November 5, 2015

Rangi ya majani yabadilika msimu wa baridi unavyokaribia karibu na ofisi za VOA Washignton DC.

Mwanajeshi wa Australia akicheza tarumbeta wakati wa maadhimisho ya miaka 100 ya mchezo wa kriketi.

Ukuta usio wa kudumu unakinga michoro ukutani kwenye sehemu inayovutia watali katika ukuta wa Berlin Ugerumani.

Wanaume waketi kwenye ubao mkubwa wa kuandikia matokeo wakati wa mechi ya kirafiki ya kriketi kati ya Zimbabwe na Bangladesh.

Wawili wapendanao wakipiga picha wakiwa kwenye daraja lililojaa taa usiku wa kuamkia sherehe za siku ya Taa mjini Seoul, Korea Kusini.

Mkazi aendesha baiskeli karibu na eneo lililokuwa na mlipuko wa bomu kwenye mji wa Douma ilioko mashariki mwa Damascus.

Waendesha pikipiki za maonyesho wakionyesha umaahiri wao kwenye ukuta maarufu 'Wall of Death' kwenye vitongoji vya mji wa Bengaluru, India.

Wanawake wafanya mazoezi ya Yoga kwenye ya kioo katika jimbo la Hunan, China.

Mwanamfalme wa Uingereza, Charles achangamshwa na nyuki alietua kwenye suruari yake na kisha kupaa wakati akishika mjusi kwenye mkono wake.

Wahandisi wa NASA kutoka kituo cha utafiti wa ndege cha Amstrong wonyesha mfano wa ndege yenye teknologia ya kupunguza utumizi wa mafuta kwa hadi asilimia 11.

Fundi wa stima aweka nyaya kwenye ukumbi wa hema New Delhi ,India.

Washinadani kwenye mchezo wa kuruka kutoka milimani wakifanya mazoezi kabla ya mashindano yatayofanyika Zhaotong kwenye jimbo la Yunnan.