Waziri wa mambo ya nje wa Norway, Borge Brende anauita utiaji saini makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Sudan Kusini “ una mashaka sana” lakini anasema inawezekana kwa nchi hiyo kurudi kwenye njia sahihi.
Baada ya mazungumzo ya jumapili katika nchi jirani ya Sudan, Brende aliliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba Sudan Kusini inahitaji mwelekeo sahihi na nyenzo za kufuatilia sitisho la mapigano.
Brende alitoa mwito wa kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kuwepo serikali ya ushirika ambayo itajumuisha kile anachokiita “makundi yote husika ya kikabila”. Wote serikali ya Sudan Kusini na waasi wanashutumiana kila mmoja kwa kukiuka mkataba wa sitisho la mapigano uliotiwa sahihi alhamis.
Mkataba huo unatakiwa kumaliza wiki kadhaa za mapigano ya silaha ambayo yalianza kati kati ya mwezi Disemba kwenye makao makuu ya jeshi kati ya makundi ya wanajeshi na wanajeshi waasi.
Rais Salva Kiir alimshutumu Makamu Rais wa zamani Riek Machar kwa jaribio la mapinduzi. Machar alikanusha madai hayo.
Norway pamoja na Uingereza na Marekani walisaidia kusimamia mkataba wa amani wa mwaka 2005 kati ya Sudan na Sudan Kusini ambao ulipelekea kupatikana uhuru kamili wa Sudan Kusini mwaka 2011.
Your browser doesn’t support HTML5