Nigeria yapokea chanjo ya Covid 19

Maafisa wa Nigeria wakipokea shehena ya kwanza ya chanjo ya Covid 19, AstraZeneca kutoka Taasisiya Cerenum, India.

Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Covid 19, Boss Mustapha amewahakikishia wanigeria wanaotaka chanjo kuwa iko salama na lengo ni kulinda afya za wananchi.

Nigeria imepokea shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya Covid 19 kutoka India. Chanjo ya Astrazeneca ni kutoka taasisi ya Cerenum ya India iliwasili mjini Abuja Jumanne usiku.

India, Umoja wa Afrika (AU) na mashirika kadhaa binafsi yametoa ahadi ya kuisaidia Nigeria katika juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Baada ya kuondolewa katika orodha ya kwanza ya nchi ambazo zitapatiwa chanjo mwezi Januari, Nigeria hatimaye imepokea shehena yake ya kwanza ya dozi milioni 4 ya Astrazeneca.

Maafisa wa Afya na Kamati ya Rais juu ya covid 19 waliungana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boss Mustapha pamoja na wanadiplomasia kadhaa kupokea chanjo hiyo kwenye uwanja wa ndege ya kimataifa wa Nnamdi Zikiwa mjini Abuja.

Boss Mustapha aliwaambia wanigeria ambao wana hamu ya kupatiwa chanjo kwamba chanjo hiyo ni salama na lengo ni kuwalinda raia dhidi ya janga la Covid.

Nigeria haitegemei chanzo kimoja cha dawa za kupambana na janga hili wakati maambukizi yameongezeka, lakini inajitahidi kutafuta misaada kutoka kwa mashirika mbali mbali ambayo yatasaidia kuipatia chanjo za kutosha kwa ajili ya watu wake takribani million 200.

Faisa Shuaibi wa Tume ya Taifa ya Afya ya Jamii anasema chanjo zaidi zina tarajiwa kuwasili mjini Abuja ikiwa ni msaada uliotolewa na Umoja wa Afrika.

Balozi wa India nchini Nigeria ambaye alijumuika na mabalozi khadhaa kupokea chanjo hiyo jumanne, Abhy Thakru amesema New Delhi imeidhinisha chanjo za ziada za AstraZeneca ambazo zitawasili Nigeria hivi karibuni.

Ripoti Imetayarishwa na Mwandishi Collins Atohengbe, Lagos, Nigeria