Netanyahu amewekewa kifaa maalum kinachosaidia mapigo ya moyo kuwa salama

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. July 5, 2023.

Madaktari wake wanasema mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 73 anatarajiwa kuruhusiwa baadaye leo. Netanyahu aliwekewa kifaa maalum cha kuangalia mapigo ya moyo wake, wiki moja iliyopita baada ya kupungukiwa na maji mwilini

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Jumapili amefanikiwa kuwekewa kifaa maalum kinachosaidia mapigo ya moyo kuwa salama (Pacemaker).

Madaktari wake wanasema mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 73 anatarajiwa kuruhusiwa baadaye leo. Netanyahu aliwekewa kifaa maalum cha kuangalia mapigo ya moyo wake, wiki moja iliyopita baada ya kupungukiwa na maji mwilini.

Taratibu zake za matibabu zinakuja wakati Israel inakabiliwa na maandamano makubwa kwa sababu ya mpango wa serikali wa kubadilisha mfumo wa mahakama wa Israeli. Kura ya mwisho juu ya marekebisho hayo imepangwa kufanyika Jumatatu.

Kama Netanyahu ataruhusiwa kutoka hospitali leo Jumapili, huenda akashiriki katika upigaji kura wa Jumatatu. Mkutano wa Jumapili wa Baraza la Mawaziri umeahirishwa.