Mpwa wake ambaye ni Mchungaji Bernice King kupitia ujumbe wa twitter ameandika kuwa shangazi yake amefariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95. Kwa miongo kadhaa tangu kuuwawa kwa ndugu yake Martin Luther King Jr 1968, Farris alishirikiana na mke wake, Coretta Scott King, katika kuhifadhi na kulinda wasia wake, ingawa mara nyingi Farris hakuwa kwenye mstari wa mbele.
Farris alizaliwa na kupewa jina Willie Christine King Septemba 11, 1927 mjini Atlanta, akiwa mtoto wa kwanza wa Mchungaji Martin Luther King Sr na mke wake Alberta Christine Williams King. Farris alisaidia Correta Scott King kujenga kituo cha The King Center na kisha akasaidia kufunza nduguye Martin Luther King Jr filosofia ya kuitisha mabadiliko bila fujo.
Kwa miaka mingi, uwepo wake ulikuwa na maana kubwa kila wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa ndugu yake kwenye kanisa la Ebenezer Baptist, ambako babu yake pamoja na baba yake waliwahi kuhubiri, na ambako Farris alibaki kuwa mfuasi.
Kituo cha King Center pia kimeandika tweet Alhamisi kikisema kwamba kinaomboleza Farris ambaye alikuwa mmoja wa wanabodi wake, wakati mmoja akiwa naibu mwenyekiti na pia mweka hazina.