Ndege za kivita za Israel zilishambulia Gaza usiku wa kuamkia Jumamosi, siku moja baada ya utawala wa Biden kuliomba bunge kuidhinisha mauzo ya makombora 45,000 kwa ajili ya vifaru vya Israel aina ya Merkava katika mashambulizi dhidi ya Hamas huko Gaza, kulingana na afisa wa sasa wa Marekani na afisa wa zamani wa Marekani.
Hatua hiyo pia inakuja siku moja baada ya Marekani kutumia kura ya turufu kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano kwasababu za kibinadamu katika vita kati ya Israel na Hamas ambalo Marekani imelitaja ni kundi la kigaidi, kidiplomasia likiitenga Washington wakati ikimlinda mshirika wake.
Bodi ya utendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inatarajiwa kukutana Jumapili kujadili hali ya afya ya Gaza. Zaidi ya nchi 12 wanachama wa WHO tayari zimeelezea wasiwasi mkubwa juu ya hali mbaya ya kibinadamu.