Mwimbaji Elton John apata mwenza.

Picha ya Elton John

Ilikuwa ni kwa kheri katika barabara ya yellowbrick, kwenye harusi iliyokuwa na shamra shamra ya mwimbaji maarufu Elton John jana jumapili.

Mwimbaji huyo wa mitindo ya rock mwenye umri wa miaka 67 ameoana na mshirika wake wa muda mrefu David Furnish karibu na London miaka tisa tangu wawili hao walipoingia katika ushirika kama mtu na mpenzi wake.

John na Furnish walioana katika sherehe za harusi ya kifahari kwenye makazi yao huko Windsor huku kukiwa na orodha ya wageni iliyojumuisha watu maarufu.

Watoto wao wawili wakiume Zachary na Elijah walibeba pete za maharusi hao.

John amesema anajivunia sana na uingereza ambako ndoa za jinsia moja hivi sasa zimekuwa halali kisheria karibu nchi nzima.

Uingereza na wales zilianza kutambua ndoa za jinsia moja mapema mwaka huu.

Scotland ilifuatia wiki iliyopita, lakini ni kuishi pamoja kwa watu wa jinsi ndiyo kunatambuliwa huko Ireland kaskazini ambako kuna wakatoliki wengi.