Mwili wa hayati Rais Jose Eduardo dos Santos kuzikwa Angola

Your browser doesn’t support HTML5

Ndege hii imeuleta nchini Angola mwili wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jose Eduardo dos Santos. Ndege hiyo iliwasili Agosti 20 jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa de Fevereiro, Luanda na kupelekwa katika makazi rasmi hayati Rais, huko Miramar, Luanda.

Kulingana na ofisi ya mawasiliano ya Rais wa Angola uamuzi wa kuurejesha mwili wake Angola umetolewa na mahakama ya Hispania kwa kuridhia maombi ya serikali ya Angola, dhidi ya matakwa ya wanawe wa kiume hayati Rais wa zamani dos Santos.

Mtoto wake ambaye alikuwa hatambuliwi na hayati Rais, alikuwa uwanja wa ndege akilia wakati akiondoka uwanjani hapo.

Ofisi ya Rais inasema kuwa taarifa zaidi kuhusu programu ya mazishi zitatolewa baadaye. Jose Eduardo dos Santos alifariki Julai 8, Barcelona, Uhispania.