Mwanahabari wa India aachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa miaka miwili

Mwanahabari Siddique Kappan aliyeachiliwa Alhamisi baada ya kuwa kizuizini kwa miaka miwili.(Photo| Facebook)

Mwandishi wa habari wa India ambaye amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka miwili bila kufunguliwa mashitaka, ameachiliwa kwa dhamana  Alhamisi,  kutokana na kesi inayomkabili ya utakatishaji pesa.

Siddique Kappan alikamatwa Oktoba 2020 katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh, ambako alikwenda kuripoti kesi nyeti ya ubakaji uliofanywa na kundi la watu wa ngazi ya juu.

Yeye pamoja na watu wengine watatu walishutumiwa kutoka kundi la kigaidi la kiislamu lenye msimamo mkali na kisha baadaye kufunguliwa mashtaka ya njama za uchochezi. Kappan amesisitiza hana hatia na kusema kwamba alisafiri kutoka jimbo lake la Kerara, ili kutekeleza majukumu yake kama mwanahabri.

Licha ya kupewa dhamana Septemba mwaka jana, Kappan aliendelea kubaki kizuizini kutokana na shutuma mpya za biashara haramu ya utakatishaji fedha dhidi yake. India imeshuka nafasi 10 kulingana na ripoti ya kundi la waandishi wasio na mipaka kwenye uhuru wa habari, tangu waziri mkuu Narendra Modi alipoingia madarakani 2014.