Mwamoyo Hamza aeleza umuhimu wa VOA kuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika wa Utangazaji

Your browser doesn’t support HTML5

Meneja wa Progamu katika Kurugenzi ya Afrika ya Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza akitoa mawazo yake kuhusu kuhudhuria mkutano mkuu wa 15 wa Umoja wa Utangazaji Afrika unaofanyika Gaborone, Botswana.⁣

Hamza amesema ni muhimu kwa VOA kuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika wa Utangazaji ili kushirikiana na watangazaji wengine. Sauti ya Amerika ilikuwa miongoni mwa wanachama wapya wa Umoja wa Afrika wa Utangazaji waliotambulishwa katika mkutano huo wa Gaborone siku ya Jumanne. ⁣