Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekataa kutia saini mswaada wenye utata dhidi ya mashoga, ambao umezungumzia adhabu ya kifo katika baadhi ya kesi, na kutaka kuwa ni vyema ufanyiwe marekebisho.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, uamuzi wa Museveni ulitangazwa Alhamisi jioni baada ya kikao cha wabunge wa chama chake tawala, ambao karibu wote waliunga mkono kuidhinishwa na wabunge mwezi uliopita.
Taarifa zimeongeza kusema kwamba wabunge hao wamekubaliana kuurejesha bungeni ili ufanyiwe marekebisho. Kwa mujibu wa video iliyorushwa na televisheni ya taifa ya UBC, Museveni anaonekana akipinga ushoga akiwa mji mkuu Kampala, akisema kwamba, “ Ulaya imepotea.
Wanataka sisi tupotee pia.” Museveni pia aliwasifu wabunge kwa kupitisha mswaada huo, ambao umezua ukosoaji mkubwa wa kimataifa.