Mugabe ateua Makamu wa Rais

Makamu wa Rais mteule wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa akiwa makao makuu ya ZANU-PF, Desemba 10, 2014.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewateua makamu wa Rais wawili kama sehemu ya mabadiliko katika chama tawala cha ZANU-PF.

Waziri wa sheria, Emmerson Mnangwagwa na mwanadiplomasia wa zamani, Pehlekezehlah Mphoko, wametajwa kuwa makamu Rais wa kwanza na wa pili, siku moja baada ya rais kumfukuza kazi makamu Rais Joice Mujuru.

Mnangagwa mshirika wa muda mrefu wa bwana Mugabe anaonekana kuwa huenda akawa mrithi wa Rais huyo wa muda mrefu mwenye umri wa miaka 90 ambaye ametawala Zimbabwe kwa miaka 34.

Bwana Mugabe amemfukuza kazi Mujuru baada ya kumshutumu kwa njama ya kutaka kumuua, shutuma ambazo mujuru amezikanusha.