Polisi wa Sudan walisema katika taarifa kwamba ufyatuaji risasi huo ni hatua ya mtu binafsi iliyokwenda kinyume na amri na kwamba taratibu za kisheria zimechukuliwa mara moja dhidi ya polisi aliyehusika.
Mwandamanaji huyo, ambaye aliuawa katika eneo la Sharg al-Nil karibu na mji mkuu wa Sudan, amekuwa mwandamanaji wa 125 kuuwawa katika maandamano ya kila wiki yaliyoanzishwa na mapinduzi Oktoba mwaka 2021.
Waandamanaji walioonekana wakiandamana kuelekea ikulu ya rais mjini Khartoum na jirani ya Omdurman walikutana na mabomu ya machozi kutoka kwa polisi, shahidi wa Reuters alisema.
Maandamano hayo yanakuja huku viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka katika mapinduzi hayo wakijadiliana makubaliano na vyama vya kiraia vilivyokuwa madarakani hapo awali ili kurejesha serikali ya kiraia.