Mtu wa pili wa kabila la Uyghur ametangazwa kufariki akiwa anashikiliwa Thailand

Mwanaharakati wa haki za binadamu anayeunga mkono wa-Uyghurs huko Hong Kong. Dec. 22, 2019.

The World Uyghur Congress ilitangaza kifo cha Mattohti Mattursun anayejulikana pia kama Muhammad Tursun hapo Aprili 24. Inasema mtu huyo mwenye miaka 40 alihamishwa kutoka kituo cha uhamiaji cha Suan Phlu mjini Bangkok hadi hospitali ya eneo hilo Aprili 21 lakini alifariki siku hiyo hiyo

Mtu wa pili wa kabila la Uyghur amefariki dunia mwaka huu kutoka miongoni mwa watu 50 au zaidi ambao Thailand imekuwa ikiwashikilia katika kituo cha mahabusu tangu mwaka 2014 licha ya wito kutoka kwa makundi ya haki za binadamu ya kutaka waachiliwe huru na kupewa makazi.

The World Uyghur Congress ilitangaza kifo cha Mattohti Mattursun anayejulikana pia kama Muhammad Tursun hapo Aprili 24. Inasema mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 alihamishwa kutoka kituo cha uhamiaji cha Suan Phlu mjini Bangkok hadi hospitali ya eneo hilo Aprili 21 lakini alifariki siku hiyo hiyo.

Mwanamme mwingine wa Uyghur anayeshikiliwa katika kituo hicho- hicho, Aziz Abdulla mwenye umri wa miaka 49, alifariki dunia Februari 11.

Wote walikuwa miongoni mwa takriban watu 50 wa jamii ya Uyghur walioachwa nchini Thailand kutoka mamia ya watu waliokamatwa wakiingia nchini humo mwaka 2014 baada ya kukimbia China ambayo Marekani na wengine wameituhumu China kwa mauaji ya kimbari kutokana na jinsi inavyowatendea Waislamu wachache, madai ambayo Beijing inayakanusha.

Wengi wao wamelazimishwa kurudi China au kurejeshwa Uturuki, mahala ambako wa-Uyghur wanadai kuwa na uhusiano na kabila la Waturuki walio wengi.