Msako waongezeka kutafuta waliopotea kwenye mafuriko Afrika Kusini

Hali baada ya mafuriko Afrika Kusini (REUTERS).

Polisi, jeshi na waokoaji wa kujitolea siku ya Ijumaa waliongeza msako wa kuwatafuta darzeni ya watu ambao bado hawajulikani walipo siku tano baada ya zaidi ya watu 340 kufariki kutokana na dhoruba mbaya zaidi kuupiga mji wa pwani wa Afrika Kusini wa Durban katika kumbukumbu ya siku za karibuni.

Mafuriko hayo yasiyokuwa na kifani, yaliathiri karibu watu 41,000, na kusababisha uharibifu mkubwa na takriban watu 341 kufariki.

Huku serikali ikiratibu shughuli ya utafutaji na uokoaji, idadi rasmi ya watu waliopotea katika jimbo la KwaZulu-Natal ilifikia 55.

Kundi la magari na helikopta zilizokuwa zimebeba wataalamu wa polisi ziliondoka mapema Ijumaa kwenda kutafuta kwenye bonde moja katika kitongoji cha Marianhill, magharibi mwa Durban, kutafuta watu 12 walioripotiwa kupotea katika mafuriko, waandishi wa AFP walisema.