Moto mjini Cairo umeteketeza studio ya Al-Ahram inayotengenezaji filamu

Watu wamekusanyika kutazama wafanyakazi wa zimamoto wakiwa kazini baada ya studio ya Al-Ahram kushika moto mjini Cairo. March 16, 2024.

Moto uliteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya studio na kusambaa hadi kwenye majengo jirani

Moto mkubwa uliozuka mjini Cairo uliteketeza moja ya nyumba za kifahari na za zamani zaidi za utengenezaji filamu katika ulimwengu wa Kiarabu, zilizoanzishwa miaka 80 iliyopita, mwandishi wa habari wa AFP alisema.

Moto uliteketeza Studio ya Al-Ahram katika wilaya ya Giza mjini Cairo, na kuchoma kila kitu kilichokuwa ndani na kusambaa hadi kwenye majengo matatu yaliyo karibu ambapo watu waliondolewa kabla ya moto huo kuwafikia.

Wakaazi wa majengo jirani walikuwa bado wamelala nje katika mitaa ya karibu na hapo, alfajiri ya Jumamosi, mwandishi wa habari wa AFP aliripoti. Ajali mbaya za moto ni kawaida nchini Misri, ambako nambari za kupiga moto unapotokea ni nadra sana kuimarishwa na idara ya huduma za dharura mara nyingi haziwasili haraka katika eneo husika.

Katika kisa hiki, vyanzo vya usalama vilisema hakuna vifo, ingawa baadhi ya watu walivuta hewa ya moshi walitibiwa katika eneo la tukio.