Moto katika jengo la ghorofa umeuwa watu 16 huko Dubai

Mfano wa jengo la ghorofa lililoshika moto huko Dubai na kusababisha vifo vya watu 16

Watu tisa walijeruhiwa katika ajali hiyo ya moto uliotokea Jumapili kulingana na maafisa huko Dubai.

Moto katika jengo la ghorofa lililopo katika moja ya vitongoji vya zamani huko Dubai umesababisha vifo vya watu 16. Watu tisa walijeruhiwa katika moto huo maafisa walisema Jumapili.

Watu wengi wanajulikana kuishi katika nyumba za jengo hilo na maeneo jirani. Ni utaratibu wa kawaida miongoni mwa vibarua wa jiji kugawanya vyumba vyao katika ukubwa wa wastani ili kusaidiana kimaisha ambapo mara nyingi hutumia mapazia ya bafuni na ubao wenye fito nyembamba mojawapo ya vitu vinavyoweza kuwa hatari kubwa ya chanzo cha moto.