Rais Mobutu Sese Seko alichukua madaraka mwaka 1965 baada ya kumpindua rais wa kwanza Joseph Kasavubu na alitawala hadi 1997.
Sehemu ya 1: Miaka ya enzi ya Mobutu Sese seko . |
Kufuatia miaka kadhaa ya uwasi na ghasia huko DRC Luteni Jenerali Joseph Desire Mobutu alichukua madaraka 1965 kwa kumpindua rais Kasavubu.
Mobutu alianzisha mfumo wa chama kimoja, na kubadlisha jina la nchi kua Zaire. Hapo akapiga marufuku vya vya kisiasa na kutawala kwa kuwakandamiza wapinzani wake wa kisiasa na wananchi. Ulaji rushwa ulikithiri na kufikia 1984 inasemekana alikua na utajiri wa dola bilioni 4 ikiwa karibu sawa na deni la taifa wakati huo, Fedha hizo zake zilikua katika akaunti yake huko Uswiss.