Mnangagwa asema wanaopinga uchaguzi wapeleke kesi mahakamani

Rais Emmerson Mnangagwa (kulia) wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi wa chama cha ZANU-PF. Picha na Zinyange AUNTONY/AFP.

Mnangagwa alipokea vyema  matokeo ya uchaguzi akisema nilishindana nao na nina furaha kwamba nimeshinda mbio hizo

Rais aliyechaguliwa tena wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema siku ya Jumapili kwamba watu wanaohoji matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao kiongozi wa upinzani alishutumu kuwa ni ya udanganyifu mkubwa wapeleke kesi yao mahakamani.

Tume ya uchaguzi ilisema Jumamosi kuwa Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80 alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 52.6 ya kura huku kiongozi wa chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC) Nelson Chamisa akipata asilimia 44%.

Mnangagwa alichukua madaraka wakati rais wa muda mrefu Robert Mugabe alipopinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2017 baada ya kukaa madarakani kwa miaka 37. Muhula wake wa kwanza uligubikwa na mfumuko mkubwa wa bei, uhaba wa fedha na ukosefu wa ajira wa kiwango cha juu.

Mnangagwa alipokea vyema matokeo ya uchaguzi akisema nilishindana nao na nina furaha kwamba nimeshinda mbio hizo alisema hayo akiwa Ikulu siku ya Jumapili huku kukiwa na wingi wa polisi katika sehemu za mji mkuu.