Mlipuko wa ugonjwa wa Kimeta umeathiri nchi tano za Afrika; inasema WHO

Bakteria aina ya Kimeta yaani Anthrax

Jumla ya visa 1,166 vya maambukizi vimeripotiwa nchini Kenya, Malawi, Uganda, Zambia na Zimbabwe. Visa 37 vimethibitishwa na vipimo vya maabara. WHO imesema Jumatatu kuwa nchi hizo tano zina milipuko ya msimu kila mwaka.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema nchi tano za Mashariki na Kusini mwa Afrika zinakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta yaani Anthrax huku zaidi ya watu 1,100 washukiwa kuambukizwa na vifo 20 vimetokea mwaka huu.

Jumla ya visa 1,166 vya maambukizi vimeripotiwa nchini Kenya, Malawi, Uganda, Zambia na Zimbabwe. Visa 37 vimethibitishwa na vipimo vya maabara. WHO imesema Jumatatu kuwa nchi hizo tano zina milipuko ya msimu kila mwaka.

Lakini Zambia ilikuwa na hali mbaya zaidi tangu mwaka 2011 na Malawi iliripoti kisa chake cha kwanza kwa binadamu mwaka huu. Uganda ilikuwa na vifo 13. Anthrax kwa kawaida huathiri mifugo kama ng'ombe, kondoo na mbuzi pamoja na mimea ya msituni.

Binadamu wanaweza kuambukizwa kama wanakaa karibu na wanyama, au bidhaa za wanyama zilizoharibika.