Mlipuko wa gari wauwa wanne Nairobi

Your browser doesn’t support HTML5

Mlipuko wa bomu ndani ya gari polisi Pangani Nairobi


Maafisa wawili wa polisi nchini Kenya na watu wengine wawili wanaodhaniwa walikua wanapanga kulipua mabomu mjini Nairobi wameuliwa baada ya gari walokua ndani kulipuka kwenye kituo cha polisi cha Pangani Nairobi.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba polisi walokuwa wanapiga doria waliona gari lilikua linaendeshwa upande usiostahiki barabarani na kulisimamisha. Baada ya kuwahoji watu wawili walokua ndani ya gari, waliamua kuwachukua pamoja na gari lao hadi kituo cha karibu cha polisi cha Pangani.

Mara baada ya kuwasili gari lilipuka na kusababisha vifo vya watu hao wanne. Shahidi mmoja karibu na tukio amiambia Sauti ya Amerika kwamba alishuhudia polisi wakiwakamata watu wawili walokua wamegeuza gari na kwnda njia isiyo stahiki.

Anasema muda mfupi baadae alisikia sauti kubwa ya mlipuko ambao polisi wanasema ulikua mkubwa na kusikika kilomita kadhaa kutoka eneo hilo.