Mlipuko wa bomu wauwa wanamgambo watano wa Palestina, Israeli yasema haihusiki na shambulizi hilo

Mlipuko wa Bomu katika eneo la mpaka wa Lebanon na Syria.

Kikundi cha wanamgambo wa Palestina cha Popular Front for Liberation kilisema wanachama wake watano waliuawa Jumatano na wengine 10 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea  karibu na mpaka wa Syria na Lebanon.

Kikundi hicho kimesema mlipuko huo ulitokea katika mji wa Qusaya na kulaumu shambulizi la anga la Israel.

Shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa wa Israel akisema jeshi la Israel halikuhusika.

PFLP imefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Israel katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita, ikiwemo kuteka nyara na kulipua ndege mbalimbali za abiria..

Marekani imekitaja kikundi hicho kuwa ni taasisi ya kigeni ya kigaidi.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.