Wamesema mitandao ya kijamii inashindwa kuwafikia takriban asilimia 45 ya wakazi, wakiongeza kwamba si zaidi ya watu milioni 600 katika bara hilo lenye jumla ya idadi ya zaidi ya watu bilioni 1.3 wana fursa ya internet.
Watangazaji hao kutoka zaidi ya mataifa 45 wamesema radio ndiyo pekee ya uhakika, inayoaminika na yenye gharama nafuu kwa wao kupata habari muhimu.
John Omo ambaye ni katibu mkuu wa Muungano wa Mawasiliano wa Afrika, ATU ameshiriki katika mkutano amesema matangazo ya radio bado yako juu juu ya aina nyingine za vyombo vya habari, ikiwemo televisheni, internet, magazeti, mitandao ya kijamii na digitali.
Ameongeza kwamba waafrika wengi hawana huduma za internet na hivyo wasinyimwe habari na mijadala ya kiuchumi, kisiasa, usalama na demokrasia kote ulimwenguni. Ameongeza kuwa Afrika ni vyema iwe na msimamo wa pamoja na kuzungumza na sauti moja katika mkutano uajo wa Duniani kuhusu mawasiliano ya radio utakaofanyika Dubai.