Mkutano wa kwanza unaoangazia hali ya hewa barani Afrika umeanza Jumatatu mjini Nairobi. Rais wa Kenya William Ruto alifungua mkutano huo wa siku tatu, baada ya kutumia gari dogo umeme baada ya kutumia msafara wa kawaida kwenda kwenye mkuntano huo, shirika la habari la Associated Press.
Bara la Afrika ambalo lina watu zaidi ya bilioni moja linaathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini linachangia kidogo katika sababu za mabadiliko. Moja ya changamoto ambazo bara hilo linakabiliana nazo katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa ni ukosefu wa rasilimali ili kukusanya takwimu za kutosha kutabiri hali ya hewa.
Katika sehemu kubwa ya dunia utabiriwa hali ya hewa ni tukio la kila siku, kuwasaidia watu kufanya maamuzi ya namna wanavyotakiwa kuvaa au wapi wanapaswa kusafiri au hata wakati gani wanapaswa kujihifadhi.
Barani Afrika, ukosefu wa utabiri wa hali ya hewa unashindwa kuwasaidia watu kufanya maamuzi ya msingi, kama vile kupanda mazao au kukimbia majanga.