Mkutano wa COP28 uwezekano wa kuleta mafanikio ni mdogo; Anasema Xie Zhenhua

Wanaharakati wa mazingira katika mkutano wa COP28 huko Dubai

Xie Zhenhua, mjumbe wa ngazi ya juu nchini China alisema chaguo jingine litakuwa kupunguza polepole vyanzo vya asili vya mafuta katika mchanganyiko wa nishati duniani.

Mjumbe wa ngazi ya juu wa China kuhusu hali ya hewa, Xie Zhenhua amesema kuna uwezekano mdogo katika mkutano wa kilele wa mabadiliko ya hali ya hewa wa COP28 utaelezewa ni wa mafanikio kama mataifa hayatakubaliana na lugha kuhusu mustakabali wa yvanzo vya asili vya mafuta.

Alipoulizwa kama China inaunga mkono nishati ya vyanzo vya asili kuondolewa, alitaja masharti yaliyotumika katika makubaliano ya “Sunnylands” yaliyofikiwa na Marekani mwezi uliopita. Alisema chaguo jingine litakuwa kupunguza polepole vyanzo vya asili vya mafuta katika mchanganyiko wa nishati duniani.

Pia alisema China inaunga mkono juhudi za kuongeza kwa mara tatu, uwezo wa nishati mbadala duniani.