Waziri wa kilimo wa Morocco ametia saini mkataba wa ushirikiano na mwenzake wa Israel Alhamisi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya kilimo na maji kati ya mataifa yote mawili.
Mkataba huo sasa unafungua njia ya kushirikiano wa timu kutoka mataifa yote mawili kufanya kazi pamoja wakati kukiwa na mpango wa kuzindua kituo cha masomo ya kilimo pamoja na miradi ya teknolojia ya kilimo na maji.
Mkataba huo umefanyika wakati wa kongamano la pili la Afya barani Afrika likifanyika, likilenga kupunguza hatari za kiafya,na ambalo limehudhuriwa na Israel mjini Marrakesh.