Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais, tawala za mikoa na Serikali za mitaa nchini Tanzania, TAMESEMI- George Simbachawene, amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wakurugenzi kutoka halimashauri za Manispaa tano katika mikoa tofauti nchini kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa.
Your browser doesn’t support HTML5
Inadaiwa kuwa wakurugenzi hao wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa ukaguzi wa hesabu kutoka ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, CAG, kwa lengo la kuandikiwa hati zisizo na dosari pindi inapobainika kuwa wana kasoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es Salaam Jumatano, waziri Simbachawene amezitaja halmashauri hizo kuwa Misenyi mkoa wa Kagera,Nanyumbu mkoa wa Mtwara, Mbogwe Geita, Kilolo Iringa na Tunduma mbeya.
Aidha Simbachawene amemvua madaraka na kuagiza mamlaka husika imsimamishe kazi ili kupisha uchungizi mkurugenzi wa halimashauri ya mji wa Tunduma, Halima Mpita , kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kuwatumia watoto wake kwenye shughuli za halimshauri na kuwalipa posho pamoja na kuisababishia Serikali upotevu wa mapato ya ushuru wa magari yanayopita kwenye mpaka wa Tunduma.