Wizara hiyo ilisema kuwa miili hiyo ilipatikana wakati wakifanya doria karibu na maeneo ya mpaka na Tunisia kati ya Dahra na Tawilat Al-Rutba.
Darzeni ya Waafrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara wamekwama karibu na mpaka wa Libya na wanasema kuwa maafisa wa Tunisia waliwaondoa na kuwaleta katika eneo hili la mpaka kutoka mji wa Sfax mapema mwezi huu.
Baadaye serikali ya Tunisia iliwahamishia kwenye makazi ya muda katika miji miwili lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yalisema kwamba darzeni ya watu bado wamekwama huko katika hali ngumu sana wameachwa na kiu na njaa katika wimbi la joto ambalo halijawahi kutokea.