Miili 21 yaopolewa katika ajali ya boti Djibouti

mashua iliyokuwa na wahamiaji inakaribia kwa operesheni ya uokoaji katika kisiwa cha Lampedusa katika bahari ya Mediterania. Walinzi wa Pwani ya Italia waliokoa watu 22 na kupata miili tisa Alhamisi, Aprili 10, 2024,

Watu kadhaa waliangamia katika maafa mapya ya boti ya wahamiaji kwenye pwani ya Djibouti, shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa lilisema Jumanne.

Ilikuwa ajali ya pili mbaya ya baharini ndani ya wiki mbili kutoka kwenye taifa hilo la Pembe ya Afrika, ambalo liko kwenye ile inayoitwa Njia ya Uhamiaji ya Mashariki kutoka Afrika hadi Mashariki ya Kati.

Meli nyingine iliyokuwa imebeba wahamiaji wengi wa Ethiopia ilizama katika eneo hilo hilo Aprili 8, na kupoteza maisha ya watu kadhaa.

Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Djibouti, Tanja Pacifico, ameliambia shirika la habari la AFP mjini Nairobi kwamba miili 21 imepatikana, huku watu 23 wakiwa bado hawajapatikana.

Watu wengine 33 walinusurika kwenye janga hilo, alisema Jumanne usiku.