Mfumuko wa bei nchini Afrika Kusini umeshuka sana kutoka kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miaka miwili mwezi Julai na kuwepo ndani ya kiwango cha benki kuu takwimu rasmi zilionyesha siku ya Jumatano.
Mfumuko wa bei wa kila mwaka wa watumiaji ulipungua hadi asilimia 4.7 mwezi uliopita ikiwa chini kutoka asilimia 5.4 mwezi Juni, shirika la takwimu la kitaifa StatsSA lilisema katika taarifa.
Hii ni rekodi ya chini kabisa tangu Juni mwaka 2021 wakati mfumuko wa bei ulipoingia kwa asilimia 4.6. Mfumuko wa bei ya chakula pia ulipungua mwezi Julai ingawa ulibaki kuwa mmoja wa wachangiaji wakubwa katika mfumuko wa bei wa jumla kwa watumiaji.
Watengeneza sera kote ulimwenguni wanapambana na mfumuko wa bei uliosababishwa kwa kiasi kikubwa na kupanda kwa bei za nishati na chakula kufuatia uvamizi wa Russia nchini Ukraine.