Shirika la habari la serikali ya Iran IRRIN limesema kwamba serikali ya Iran imepata idhini ya mahakama ya kushikilia meli ya mafuta ya Bahamas kwa jina Richmond Voyager, baada yake kugongana na ile ya Iran kwenye Ghuba ya Oman.
Jeshi la wanamaji la Marekani limesema kwamba limeingilia kati ili kuzuia Iran kushikilia meli mbili kwenye Ghuba hiyo.
Kulingana na ripoti iliyotangazwa na IRRIN kutoka kituo utafutaji na uokozi wa baharini kwenye jimbo la Hormozgan Iran, meli hiyo ya Bahamas iligongana na ile ya Iran iliyokuwa na wanabaharia 7, wakati watano kati yao wakijeruhiwa vibaya.
Takriban meli moja kwa kila 5 za mafuta ulimwenguni hutumia mfereji wa Hormuza ulioko baharini kati ya Iran na Oman kwa mujibu wa takwimu kutoka kampuni ya Vortexa.