Mdahalo kati ya Harris na Trump wajikita katika vita, uhamiaji, uchumi na utoaji mimba

  • VOA News

TOPSHOT - Mgombea Urais Kamala Mdemokrat Kamala Harris (kulia) akimsalimia mpinzani wake mgombea urais wa Republikan Donald Trump kabla ya kuanza Mdahalo wa Rais katika kituo chaNational Constitution Center huko Philadelphia Jumanne usiku,

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, alikabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic, Kamala Harris, katika mdahalo uliofanyika jana Jumanne, kuhusu masuala kama vile utoaji mimba, uhamiaji na sera za kigeni.

Mdahalo huo uliowakutanisha ana kwa ana kwa mara ya kwanza, kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Novemba.

Jukwaa liliandaliwa kwa kile ambacho huenda ikawa ni muda muhimu wa kampeni kuelekea uchaguzi wa rais wa Marekani Novemba 5.

TOPSHOT - Mgombea urais Donald Trump wakati wa mdahalo na Makamu wa Rais Kamala Harris katika kituo cha National Constitution Center huko Philadelphia, Pennsylvania, on September 10, 2024.(Photo by SAUL LOEB / AFP)


Wagombea hao wawili hawajawahi kukutana au hata kuzungumza kwa simu, lakini Jumanne walisimama umbali mdogo kati yao nyuma ya kizimba katika National Constitution Center huko Philadelphia.

Malumbano hayo yalidumu kwa dakika 90 na yaliyoendeshwa watangazaji wawili wa kituo cha televisheni cha ABC, David Muir na Linsey Davis.⁣

Mdahalo huu kati ya wagombea wa urais kwa kile kinachoweza kuwa ni mdahalo wa kipekee wa kampeni hii.

Tukio hili limefanyika wiki nane kabla ya siku Rasmi ya Uchaguzi lakini siku chache tu kabla ya upigaji kura wa mapema utaanza katika baadhi ya majimbo 50 ya nchi hii.