Mchezaji Kubi Banga wa Burundi auwawa

Mchezaji wa kandanda wa Burundi Kubi Banga

Inasemekana watu wasiojulikana walimpiga panga la kichwa baada ya kuhudhuria tafrija ya ushindi kwa timu yake ya Lydia Lydic Academie
Mchezaji maarufu wa kimataifa katika mpira wa soka nchini Burundi ameuwawa Alhamis usiku huko mjini Bujumbura.

Kubi Bangi Lewis wa timu ya soka ya Lydia Lydic Academie iliyotwaa ubingwa kwa mwaka wa pili mfululizo nchini humo aliuwawa na watu wasiojulikana kwa kupigwa panga kichwani baada ya kuhudhuria tafrija iliyoandaliwa juu ya ushindi huo.

Marafiki wanaomfahamu walimuelezea Lewis kuwa ni mtu aliyekuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wenzake na kifo chake ni pigo kwa familia, wanamichezo, na taifa kwa jumla.

Timu hiyo itaiwakilisha Burundi kwenye mashindano ya kombe la shirikisho la Afrika.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Amida Issa, Bujumbura