Mazungumzo ya usitishaji mapigano nchini Sudan yanayosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani yanaonekana kukwama tena

Jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa linaonekana kutoka ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu, Septemba 21, 2021.

Mazungumzo ya usitishaji mapigano nchini Sudan yanayosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani yanaonekana kukwama tena, huku jeshi la taifa la nchi hiyo na kikosi cha dharura cha RSF vikiendelea na mapigano kati yao. Mapigano hayo yanaendelea kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu nchini humo.  

Kutopatikana kwa maendeleo kwenye mazungumzo ya Jeddah kumesababisha matumaini kutoweka ya kupatikana suluhu kwa mzozo ambao umesababisha zaidi ya watu milioni 6.5 kukosa makazi yao nusu wakibaki ndani ya nchi na wengine kukimbilia nje, pamoja na kuangamiza uchumi wa nchi na kuzusha upya mapigano na mauwajiu ya kikabila katika jimbo la magharibi la Darfur. Jeshi la Sudan limeongeza matamshi yake makali ya kuendelea na vita, huku wakazi wakisema kwamba mashambulio ya anga yameongezeka katika mji mkuu wa Khartoum, huku wapinzani wao RSF wakiendelea kuteka sehemu za majimbo ya Darfur na kordofan.