Mawaziri hao walikutana Cameroon mwishoni mwa wiki, nakusema nchi hizo tatu kwa pamoja zitaungana kupambana na ukosefu wa usalama kutoka kwenye bandari ya Douala, Cameroon.Wameongeza kusema kwamba walikwenda kutafuta suluhisho la haraka kwa vikwazo vinavyokabili usafirishaji wa bidhaa kutoka Cameroon katika bandari za Douala na Kribi kuelekea kwenye mataifa ya Afrika ya Kati ambayo hayana bahari.
Bandari hizo zinashughulikia asilimia 90 ya bidhaa zinazopelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad na CAR zinasema mwezi uliopita polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya raia katika miji na vijiji kadhaa wakati wakilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa. Kuna karibu asilimia 35 ya ongezeko la bei za vyakula, serikali mbili zinasema.
Cameroon, Chad na CAR, pia zimesema zitavunja zaidi ya vituo 70 vya ukaguzi ambavyo wanasema vilanzishwa kinyume cha sheria na polisi wa Cameroon, pamoja na jeshi kwenye njia kati ya Douala na N’djamena.
Katika ujumbe wao wa mwaka mpya marais Mahamat Idriss Deby wa Chad, na Faustin-Archange Touadera wa CAR wameomba msaada wa dharura wa chakula kwa ajili ya takriban watu milioni tano ambao wanasema wanakabiliwa na njaa, pamoja na ujosefu wa usalama wa chakula.