Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte leo Ijumaa alifungua siku ya pili ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa muungano huo walipokutana mjini Brussels kujadili masuala ya kimataifa ikiwemo vita vya Ukraine.
Katibu Mkuu alisema Muungano huo unaongeza kwa kiasi kikubwa msaada kwa Ukraine kwa ulinzi wake sasa na katika siku zijazo.
Pia aliangazia mipango ya kuongeza uwezo wa viwanda vya ulinzi, uzalishaji na minyororo ya usambazaji kote katika Muungano.
Maoni hayo yalitolewa leo Ijumaa kabla ya kikao cha faragha.
Siku ya Alhamisi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alikutana mjini Brussels na viongozi wa Umoja wa Ulaya na kisha mawaziri wa ulinzi wa NATO kujadili mpango wake wa kumaliza vita vikali vya nchi hiyo na Russia.
Mpango huo unalenga kuifanya Russia kumaliza mgogoro kwa njia ya mazungumzo.