Machi mwaka huu serikali ilifunga mitandao ya Facebook, TikTok, Telegram na YouTube, kote nchini kufuatia kutoelewana na kanisa la ki Orthodox chini, ambalo baadhi ya viongozi wake walikuwa wanaitisha maandamano. Hata hivyo baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kama vile Amnesty International yamesema kwamba marufuku hiyo inahujumu haki ya kujieleza, na ni kunyume cha katiba ya Ethiopia, sheria pamoja na mikataba ya kimataifa.
Kupitia taaarifa naibu mratibu wa Amnesty mashariki na kusini mwa Afrika Flavia Mwangonya ameongeza kwamba hatua hiyo inaweka doa kwenye rekodi yenye mashaka ya uhuru wa vyombo vya habari nchini humo. Licha ya kwamba baadhi ya watu wanaweza kutumia mitandao ya kibinasfi ya VPN, bado ni vigumu kufikia wafuasi au wateja wao ndani ya nchi.